Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » KAMA KAWAIDA YAO WASIVYO CHELEWA,TAYARI WAMESHA MNASA HUYU KIFAA WA ZAMANI WA BAYERN MUNICH.

KAMA KAWAIDA YAO WASIVYO CHELEWA,TAYARI WAMESHA MNASA HUYU KIFAA WA ZAMANI WA BAYERN MUNICH.

Written By Unknown on Monday, 7 July 2014 | Monday, July 07, 2014

Hatimaye mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid wamewashiwa taa ya kijani katika mbio za kumsajili kiungo kutoka nchini Ujerumani na klabu ya FC Bayern Munich, Toni Kroos.
Kwa mujibu wa gazeti la Marca, klabu ya Real Madrid wamewashiwa taa ya kijani kumsajili Kroos, kufuitia ofa yao kuwavutia mabosi wa klabu ya FC Bayern Munich, ambao pia walipokea ofa kutoka kwenye klabu nyingine kama Man utd na Chelsea zote za nchini Uingereza.
Viongozi wa Real Madrid wameripotiwa kuwasilisha ofa ya paund million 25, ambayo ni tofauti na ofa nyingine zilizotua huko Allianz Arena mjini Munich.
Gazeti hilo limeendelea kusisitiza kwamba taratibu za usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, zitafanyika mara baada ya fainali za kombe la dunia zinazoendelea huko nchini Brazil.
Toni Kroos, kwa sasa yupo nchini Brazil akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani akijiandaa na mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya wenyeji ambao umepangwa kufanyika kesho.


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi