Shirika la usafiri wa anga la Tunisia limefuta safari zake za ndege
katika miji ya Tripoli na Misrata huko Libya. Shirika la usafiri wa
ndege la Tunisia limeamua kufuta safari zake katika miji hiyo kufuatia
kuendelea mapigano kati ya makundi ya wanamgambo wenye silaha huko
Tripoli kwa lengo la kuudhibiti uwanja wa ndege wa kimataifa wa mji
huo. Shirika la ndege la Tunisia limesimamisha safari zake katika miji
iliyotajwa tangu jana Jumanne. Mashambulizi ya makundi ya wanamgambo
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tripoli yameusababishia hasara
uwanja huo na vile vile majengo ya karibu yake.
Home »
siasa afrika
» SAFARI ZA MISRATA PAMOJA NA TRIPOLI ZAFUTWA NA SHIRIKA LA USAFIRI WA ANGA LA TUNISIA.
SAFARI ZA MISRATA PAMOJA NA TRIPOLI ZAFUTWA NA SHIRIKA LA USAFIRI WA ANGA LA TUNISIA.
Written By Unknown on Wednesday, 16 July 2014 | Wednesday, July 16, 2014
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!