Ahmet Davutoğlu ambaye alikuwa akizungumza na vyombo vya habari amesema mashambulizi ya Israel huko Ghaza hayawezi kutetewa kwa njia yoyote ile na kuongeza kuwa Israel imeamua kutekeleza mashambulizi hayo katika kipindi cha sasa ambapo nchi za Kiislamu zimedhoofika na inatumia fursa hiyo kuwanyanyasa raia wa Palestina.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amesema kuwa mashambulizi ya Israel hayawezi kuvunja azma ya Wapalestina ya kuunda nchi huru na kwamba Israel inafanya makosa iwapo inadhani kwamba kwa kuwaua Wapalestina na kuliangamiza kundi la Hamas inaweza kuyaweka madarakani makundi yanayoiunga mkono huko Palestina.
Wakati huo huo mashambulizi ya kinyama yanayoendelea kufanywa na jeshi la utawala wa kigaidi wa Israel kwa siku ya kumi sasa katika Ukanda wa Ghaza yameendelea kulaaniwa na nchi na jumuiya mbalimbali za kimataifa. Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa idadi kubwa ya waliouawa katika mashambulizi ya Israel huko Ghaza ni raia wa kawaida na kwamba nusu ya majeruhi ni wanawake na watoto wadogo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!