Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , , , » BAADA YA FUTURE NA CIARA HAWA NI WENGINE WAKALI KUTOKA MAREKANI AMBAO WAMETANGAZA KUACHANA.

BAADA YA FUTURE NA CIARA HAWA NI WENGINE WAKALI KUTOKA MAREKANI AMBAO WAMETANGAZA KUACHANA.

Written By Unknown on Friday 22 August 2014 | Friday, August 22, 2014

Mchekeshaji Nick Cannon amethibitisha kuwa yeye na mkewe Mariah Carey walitengana miezi kadhaa iliyopita na kwamba hakuna maelewano tena katika nyumba yao.
Nick amemwambia mtu wa ndani wa E! kuhusu hilo huku akificha maelezo ya chanzo cha kutengana kwao na kwamba hivi sasa anafikiria zaidi kuhusu watoto wao mapacha wenye umri wa miaka mitatu.
“Hivi sasa, focus yangu kubwa ni kwa watoto wangu.” Ameeleza.
Taarifa zinaeleza kuwa chanzo cha ugomvi wao ni pale ambapo Nick Cannon alipofanya mahojioano na Power 106 na kueleza kuhusu maisha yake ya nyuma katika uhusiano na wasichana aliowahi kutoka nao.
Nick alieleza hewani kuwa aliwahi kutoka na wasichana wengi maarufu, wanamuziki na wanamitindo na miongoni mwao akawataja Christina Milian na Kim Kardashian.
Mbali na hapo aliitaja siku ya kwanza kufanya mapenzi na Mariah Carey ambapo alidai kuwa alipewa sharti la kufunga ndoa kwanza ndipo mengine yaendelee. Hivyo alilichuma tunda la mkewe kwa mara ya kwanza usiku baada ya kufunga pingu za maisha.
Maelezo hayo ndio mwiba uliochoma uhusiano wake na kuleta mvurugano huku ikielezwa kuwa Mariah alianza kumtumia hadi walinzi kumlinda dhidi ya wasichana alipokuwa katika kazi zake za ushereheshaji.
Inaripotiwa kuwa wawili hao tayari wameshafanya makubaliano ya talaka na taratibu zinaendelea ila kila mmoja aendelee na maisha yake.
Nick Cannon na Mariah Carey wafunga ndoa mwaka 2008 wiki chache baada ya kutangaza uhusiano wao rasmi.

 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi