Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , , » DIAMOND HATAREEE,AWEKA HADHARANI KIWANGO ANACHO KISHIKA KWA SASA KWENYE SHOW NDANI NA NJE YA TANZANIA,MTAWEZA?

DIAMOND HATAREEE,AWEKA HADHARANI KIWANGO ANACHO KISHIKA KWA SASA KWENYE SHOW NDANI NA NJE YA TANZANIA,MTAWEZA?

Written By Unknown on Friday 22 August 2014 | Friday, August 22, 2014

Tangu mwaka juzi tulifahamu kuwa Diamond Platinumz ndiye msanii pekee kutoka nchini Tanzania anaelipwa kiasi kikubwa cha pesa, na mwaka jana ikaelezwa kuwa bila milioni 10 au 8 za Kitanzania humpati kwenye show yako.
Lakini kiwango kipya kilichotajwa jana kitawapa kizunguzungu zaidi hasa mapromota wenye mitaji midogo wenye ndoto za kufanya kazi na mwimbaji huyo.
Kwa mujibu wa, Babu Tale ambaye ni meneja wake, hivi sasa kiwango cha chini anachochaji kwa show moja hapa nchini ni $15,000 (sawa na shilingi Milioni 25 za Burundi).
“Tuna show Marekani show kumi na tano (15), show kumi na tano dola elfu ngapi? Na kwa hapa Tanzania hatufanyi show chini ya dola e15,000.”  Babu Tale alisema.
Kwa mujibu wa Babu Tale, wanachaji kiasi cha hadi dola 25,000 kwa show moja za nje ya nchi (ikiwemo Marekani).
Tunalipwa milioni 20 show moja, tunalipwa dola elfu 25,000 show moja, hii ni zaidi ya madawa ya kulevya.” Alisema wakati akikanusha tuhuma kuwa Diamond anauza dawa za kulevya.
Kwa mahesabu ya haraka haraka, shows 15 mara dola 25,000 ni sawa na  $375,000 (Sawa na shilingi za Tanzania 625,687,500).
Yesss! Ni zaidi ya Milioni mia sita ishirini na tano za kitanzania.
Kama ni kweli, basi Diamond anastahili kweli kuitwa Dangote wa Bongo Flava.
Bado michongo inaendelea kumiminika ambapo hivi karibuni meneja wa Trey Songz alimtumia ujumbe kuwa atakapokuwa na nafasi amshitue waongee.



TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi