Club ya Arsenal ya Uingereza wamelazimisha suluhu pacha ya bila kufungana na Besiktas ya Uturuki
katika mchezo wa kwanza wa mtoano wa ligi ya mabaingwa barani Ulaya
uliopigwa jana usiku katika dimba la Ataturk Stadium
Kutoka
sekunde za mwanzo, almanusura Demba Ba afunge bao lakini mpira aliopiga
wa adhabu ndogo uligonga mwamba na ilionekana kuwa ni mechi ambayo
ingekuw ana magoli mengi. Lakini Aaron Ramsey naye aliwakosa Waturuki hao baada ya kupiga shuti lililogonga mwamba.
Kadi
nyekundu ya Aaron Ramsey aliyopata dakika za majeruhi kufuatia
kuoneshwa kadi mbili za njano aliwahuzunisha zaidi Asernal kutokana na
ukweli kuwa anahitajika sana katika mchezo wa marudiano ndani ya dimba
la Emitarates.
Kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey alitolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo wa kwanza wa mtoano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Besiktas |
Besiktas,
na Ba wameonekana kuwa na nia ya kuwaonesha Chelsea kuwa walifanya
makosa kumuuza mshambuliaji huyo kwani alionesha kiwango kizuri. Ili
kusonga mbele, Asernal wanahitaji ushindi wa bao 1-0 tu mjini London
jumanne ijayo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!