Siku kama ya leo miaka 61 iliyopita kulifanyika mapinduzi ya Kimarekani
dhidi ya serikali ya Dakta Muhammad Musaddiq nchini Iran na baadaye
kidogo Shah Reza Pahlavi akatwaa tena madaraka ya nchi. Mapinduzi hayo
ambayo yalipangwa na shirika la ujasusi la Marekani CIA kwa ushirikiano
wa Uingereza, yaliiondoa madarakani serikali ya Musaddiq kupitia njia ya
kuzusha hitilafu na mifarakano kati ya wanaharakati wa kisiasa na
wananchi na kueneza anga ya ghasia na machafuko nchini Iran. Vilevile
yalimrejesha Iran Shah Pahlavi ambaye siku tatu kabla alikuwa
amekimbilia nchini Italia.
Kabla ya tukio hilo la kusikitisha, wananchi Waislamu wa Iran walikuwa wamefanikiwa kukata mkono wa Uingereza nchini Iran na kutaifisha sekta ya mafuta iliyokuwa ikidhibitiwa na wakoloni hao.
Kabla ya tukio hilo la kusikitisha, wananchi Waislamu wa Iran walikuwa wamefanikiwa kukata mkono wa Uingereza nchini Iran na kutaifisha sekta ya mafuta iliyokuwa ikidhibitiwa na wakoloni hao.
***********************************************
Siku kama ya leo miaka 352 iliyopita
alifariki dunia Blaise Pascal, mwandishi, mwanahesabati na mvumbuzi wa
mashine ya kuhesabia (calculator) wa Kifaransa. Alizaliwa Juni mwaka
1623 na tangu utotoni Pascal alivutiwa mno na somo la hesabati. Vilevile
urafiki uliokuwepo kati ya baba yake Pascal na msomi mmoja maarufu wa
zama hizo ulisaidia mno katika kuchanua kipawa na kugunduliwa uwezo wa
kijana huyo katika taaluma ya hisabati. Mwishoni mwa umri wake Blaise
Pascal alijielekeza mno katika masuala ya dini na kuandika vitabu kadhaa
katika uwanja huo.
***********************************************
Na miaka 23 iliyopita katika siku kama ya leo
makamanda wa ngazi za juu wa jeshi la Urusi ya zamani wakiongozwa na
Gennadi Ivanovich Yanayev walifanya mapinduzi dhidi ya rais wa mwisho wa
Muungano wa Sovieti Mikhail Gorbachev. Wanajeshi hao walitaka
kukomeshwa marekebisho ya Gorbachev na kuzuia mpango wa kugawanywa Urusi
ya zamani. Wakati wa mapinduzi hayo Mikhail Gorbachev alikuwa katika
Peninsula ya Crimea huko kaskazni mwa Bahari Nyeusi. Hata hivyo Boris
Yeltsin ambaye wakati huo alikuwa kiongozi wa Federesheni ya Urusi na
ambaye alikuwa akiungwa mkono na Magharibi, alizima mapinduzi hayo kwa
msaada wa wananchi na baadhi ya watu wenye ushawishi serikalini.
Kushindwa kwa mapinduzi hayo kulizidisha uwezo na satua ya Boris Yeltsin
na kuharakisha mwenendo wa kusambaratika Urusi ya zamani hapo mwaka
1991.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!