Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amekosoa vikali kimya cha jamii ya
kimataifa kuhusiana na mashambulio ya kinyama ya utawala haramu wa
Israel pamoja na jinai za utawala huo dhidi ya wananchi wa Palestina.
Rais Mugabe ambaye ni mwenyekiti wa kiduru wa Jumuiya ya Ustawi ya
Kusini mwa Afrika SADC amebainisha kwamba, kimya cha jamii ya kimataifa
kuhusiana na jinai hizo za Israel hakuna tofauti na kutenda jinai. Rais
Mugabe amesema, madola ya magharibi yanayojifanya kuwa vinara katika
masuala ya maadili, haki za binadamu na wanadamu kamili yamekuwa
watazamaji tu wa mauaji ya umati ya Israel dhidi ya wanawake na watoto
wasio na hatia wa Palestina. Rais Mugabe wa Zimbabwe amesisitiza juu ya
jumuiya ya SADC kufungamana na taifa la Palestina na kuongeza kuwa, imma
Israel ni muhimu mno kwa Wamagharibi ndio maana hawawezi kuzuia jinai
za utawala huo, au watoto wadogo wanaouawa kwa umati huko Gaza ni
magaidi.
Home »
siasa afrika
,
siasa kimataifa
» KAMA ULIKUWA HAUJUI HUYU NDIE RAIS SHUPAVU,SOMA VILE ALIVYO IKOSOWA JAMII YA KIMATAIFA KUHUSU MACHAFUKO YANAYO ENDELEA KUFANYWA NA ISRAEL KWA WAPALESTINA HUKO GAZA.
KAMA ULIKUWA HAUJUI HUYU NDIE RAIS SHUPAVU,SOMA VILE ALIVYO IKOSOWA JAMII YA KIMATAIFA KUHUSU MACHAFUKO YANAYO ENDELEA KUFANYWA NA ISRAEL KWA WAPALESTINA HUKO GAZA.
Written By Unknown on Wednesday, 20 August 2014 | Wednesday, August 20, 2014
Labels:
siasa afrika,
siasa kimataifa
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!