Klabu ya Arsenal imepiga hatua nzuri katika mbio za kumsajili beki wa Olympiacos Kostas Manolas. Meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger anataka kusaini beki mpya kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa kiangazi kufuatia kuondoka kwa nahodha wake Thomas Vermaelen kwenda Barcelona.
Arsenal kwasasa ina uhaba wa mabeki kufuatia kuumia msuli kwa Kieran Gibbs ambapo atakaa nje kwa kipindi cha wiki tatu zijazo. Wenger kwasasa anafanya kila njia kuhakikisha anakamilisha usajili huo ambao unaweza kumgharimu paundi milioni 6.5 kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo Septemba mosi.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!