Home »
siasa afrika
» HABARI KUTOKA LIBYA ZASEMA KUWA MAWAZIRI WA NCHI JIRANI NA NCHI HIYO WAKUTANA JIJINI CAIRO MISRI.
HABARI KUTOKA LIBYA ZASEMA KUWA MAWAZIRI WA NCHI JIRANI NA NCHI HIYO WAKUTANA JIJINI CAIRO MISRI.
Misri leo inatazamia kuwa mwenyeji wa kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje
wa Libya wa nchi jirani zake. Wizara ya Mambo ya Nje ya Libya
imetangaza kuwa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Libya, Misri, Tunisia,
Algeria, Sudan, Chad na Niger wanatazamiwa kushiriki katika kikao hicho
cha Cairo.
|
Hapa ni Cairo nchini Misri... |
Kundi hilo la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi hizo
zilizotajwa mwezi uliopita lilifanya kikao na kutaka kufanyika
mazungumzo ya kisiasa na kuundwa baraza la kufuatilia ufumbuzi wa
mgogoro wa Libya. Hii ni katika hali ambayo, kundi la Fajr la huko Libya
jana lilitangaza kuwa linadhibiti uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Tripoli. Libya imekuwa ikikabiliwa na hali ya mchafukoge na mapigano ya
ndani miaka mitatu baada ya kupinduliwa kiongozi wa nchi hiyo Kanali
Muammar Gaddafi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!