Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » JE,ULISIKIA KILE WALICHO KISEMA BOKO HARAMU?BASI HIKI HAPA KISOME NA WEWE...

JE,ULISIKIA KILE WALICHO KISEMA BOKO HARAMU?BASI HIKI HAPA KISOME NA WEWE...

Written By Unknown on Monday, 25 August 2014 | Monday, August 25, 2014

Wanamgambo wa kitakfiri wa kundi la Boko Haram wa nchini Nigeria wametangaza kuasisi kile walichokitaja kuwa ni utawala wa Khilafa huko kaskazini mashariki mwa mji wa Gwoza. Abubakar Shekau  kiongozi wa kundi la Boko Haram amesema katika mkanda wa video wa dakika 52 kuwa, ameasisi utawala wa Kikhalifa katika mji wa Gwoza baada ya kuuteka mapema mwezi huu.
Kiongozi wao mkuu Bwana Abubakar Shekau akiwa mbele...
Shekau ameongeza kuwa yeye na wanamgambo wa kundi la Boko Haram wamekuja kuishi katika mji huo na kwamba hawakusudii kuondoka katika mji huo. Hata hivyo jeshi la Nigeria kwa upande wake limepinga madai ya kiongozi huyo wa Boko Haram juu ya kuuteka mji wa Gwoza. Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Nigeria amesema madai ya Boko Haram ni ya uwongo.  
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi