Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , , , » SHEREHE AMBAZO MWANAMUZIKI C.BROWN ALIKUWA MSHEREHESHAJI ZILIINGILIWA NA DOSARI BAADA YA SUGE KNIGHT KUPIGWA RISASI 6.

SHEREHE AMBAZO MWANAMUZIKI C.BROWN ALIKUWA MSHEREHESHAJI ZILIINGILIWA NA DOSARI BAADA YA SUGE KNIGHT KUPIGWA RISASI 6.

Written By Unknown on Monday 25 August 2014 | Monday, August 25, 2014

Party ya utangulizi wa utoaji tuzo za video za MTV (Pre-VMA Party) iliingia dosari baada ya CEO wa zamani wa Death Row Records alikuwa mmoja kati ya watu watatu waliojeruhiwa vibaya kwa risasi.
Kwa mujibu wa TMZ, machafuko hayo yalitokea nje ya club ya usiku ya 10AK magharibi mwa Hollywood majira ya saa saba na nusu usiku.
Suge Knight anaripotiwa kupigwa risasi sita zilizompata tumboni, mkononi na sehemu nyingine za mwili. Alikimbizwa hospitali ambapo hali yake inaripotiwa kutia matumaini baada ya kufanyiwa upasuaji.
Polisi walifika katika club hiyo na watu wote walitoka wakiwa wameweka mikono juu kufuatia tukio hilo la hatari.

Chris Brown alikuwa mshereheshaji katika party hiyo ambayo ilihudhuriwa na watu maarufu akiwemo Tyson Beckford.
Mashuhuda wameeleza kuwa kabla ya tukio hilo, rapper The Game na rafiki zake waligombana na mlinzi wa club hiyo na kukataliwa kuingia ndani. Game aliondoka na kuwaacha rafiki zake maeneo hayo.
Kufuatia tukio hilo,  Polisi wanafanya uchunguzi dhidi ya makundi mawili ya kihalifu ambayo yalikuwa na beef ya muda mrefu. Game na Suge Knight wote wanahusishwa na kundi maarufu la bloods.
“It's disappointing that we as a society can't have fun or enjoy ourselves without any altercations sometimes. Miss me with the bullshit!!!” Alitweet Chris Brown baada ya tukio hilo.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi