Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imethibitisha wagonjwa wawili wa
wa kwanza kuambukizwa ugonjwa wa ebola nchini humo, na hivyo Kongo
kuwa nchi ya tano ya Kiafrika kuthibitisha kesi za homa hiyo hatari.
Felix Kabange Numbi Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
amesema kuwa taasisi ya taifa ya utafiti wa kitiba ya nchi hiyo
imethibitisha kuwa sampuli mbili za uchunguzi wa kimaabara za wagonjwa
hao zimeonyesha kuwa watu hao wameambukizwa virusi vya homa hatari ya
ebola.
Kabange amesema huo ni mlipuko wa saba wa homa ya ebola kuwahi kuikumba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kwamba uzoefu ulioupata nchi hiyo katika milipuko sita iliyopita ya maradhi hayo, utatumika ili kukabiliana na maambukizo ya homa hiyo.
Shirika la Afya Duniani (WHO) jana lilisema kuwa mtaalamu wake wa magonjwa ya milipuko aliyekuwa ametumwa na shirika hilo huko magharibi mwa Afrika kwa minajili ya kutafuta njia za kukabiliana na mlipuko wa ebola ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo. Hadi kufikia sasa watu 1427 wamefariki dunia kwa homa hatari ya ebola huko magharibi mwa Afrika.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!