Kurejea kwa mshambuliaji kutoka nchini Italia Super Mario Barwuah
Balotelli katika ligi ya nchini Uingereza baada ya kusajiliwa na majogoo
wa jiji Liverpool, hakujamshtua meneja wa klabu bingwa nchini humo
Manuel Luis Pellegrini Ripamonti.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliokuwa na mlengo wa mchezo wa hii leo, Manuel Pallegrini amesema hatua ya kurejea kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, anaichukulia kama ilivyo usajili wa wachezaji wengine waliojiunga na klabu zinazoshiriki ligi ya nchini Uingereza.
Amesema hakuna asiyejua Balitelli alikuwepo Man city na kisha alirejea nyumbani kwao Italia na akajiunga na AC Milan na sasa amerejea tena nchini Uingereza, hivyo kwa nini ichukuliwe kama ni mshangao kwake? Alihoji mzee huyo kutoka nchini Chile.

Pellegrini pia akaizungumzia tabia ya Mario Balotelli kwa kuwaeleza
waandishi wa habari kwamba anamfahamu vyema na amekuwa na wasifu wa
kipekee hivyo haoni la ajabu zaidi.
Ikumbukwe kuwa hii leo ligi ya nchini Uingereza itaendelea tena kwa
mchezo mmoja ambapo Man city watakuwa nyumbani Etihad Stadium wakicheza
dhidi ya majogoo wa jiji Liverpool waliomrejesha Super Mario Barwuah
Balotelli nchini Uingereza kwa ada ya uhamisho wa paund million 16
akitokea AC Milan ya nchini Italia.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!