Amani na utulivu vimerejea sasa huko Msumbiji baada ya mapigano
ya miaka miwili kati ya serikali ya Msumbiji na wapinzani. Serikali ya
Msumbiji na chama kikuu cha upinzani cha Renamo jana vilisaini
makubaliano ya kusimamisha mapigano. Jose Pacheco Waziri wa Kilimo wa
Msumbiji ambaye ni afisa mwandamizi katika timu ya mazungumzo ya
serikali na Saimone Macuiana mwakilishi wa timu ya mazungumzo kwa upande
wa waasi wa Renamo jana walisaini makubaliano ya kusitisha mapigano
baada ya mazungumzo ya masaa sita.
Afisa mwandamizi wa timu ya mazungumzo ya waasi wa Renamo amesema kuwa kutiwa saini makubaliano hayo ni sawa na kumalizika uhasama kati ya Renamo na serikali ya Maputo. Macuiana ameongeza kuwa, ukurasa mpya umefunguliwa huko Msumbiji kwa kufikiwa makubaliano hayo na kwamba nchi hiyo hiyo imeingia katika kipindi kipya. Itakumbukwa kuwa chama tawala cha nchini Msumbiji Frelimo na chama cha upinzani Renamo tarehe 11 mwezi Agosti mwaka huu vilisaini makubaliano ya awali huko Maputo mji mkuu wa nchi hiyo kwa lengo la kukomesha machafuko nchini humo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!