Vikosi vya usalama vya Somalia vimemtia
mbaroni mmoja wa viongozi wa maharamia wa nchi hiyo wenye nguvu, ambaye
alikuwa akiziteka nyara meli kubwa katika pwani ya Somalia. Kiongozi
huyo wa maharamia wa Somalia alikuwa akijipatia mamilioni ya dola
kupitia fedha alizokuwa akilipwa kama kikomboleo. Duru za usalama za nje
na za ndani ya Somalia zimetangaza kuwa vikosi vya usalama vya Somalia
jana usiku vilimtia mbaroni Mohamed Garfanji pamoja na walinzi wake
kadhaa huko Mogadishu mji mkuu wa nchi hiyo.
Rais Hassan Sheikh Mahmoud wa Somalia
mwaka jana alitoa msamaha kwa maharamia wa nchi hiyo ili kukomesha
mashambulizi yao karibu na pwani ya nchi hiyo ya eneo la Pembe ya
Afrika, hata hivyo alisema kuwa msamaha huo hauwahusu viongozi wa
mtandao huo. Imeelezwa kuwa Mohamed Garfanji amekamatwa katika
oparesheni moja ya upokonyaji silaha na kwamba ametiwa mbaroni si kwa
sababu ya uharamia.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!