Mkuu wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(Monusco) hajapinga uwezekano wa
kutumiwa njia ya kijeshi dhidi ya waasi wa Rwanda wa FDLR huko mashariki
mwa nchi hiyo. Martin Kobler amesema amewataka waasi wa Rwanda kujiunga
kwa khiari na mchakato wa kuweka chini silaha zao. Afisa huyo wa Umoja
wa Mataifa amesema kuwa kikosi cha kulinda amani cha umoja huo(Monusco)
na jeshi la Kongo vitalazimika kutumia njia ya kijeshi iwapo ombi hilo
kwa waasi wa FDLR halitatekelezwa.
Wakiwa mkutano huko Angola wiki iliyopita,wakuu wa nchi za eneo za Maziwa Makuu ya Afrika pia walitaka kupokonywa silaha waasi hao wa Rwanda na kukaribisha kurejea nchini kwao baadhi ya waasi hao.
Mwenendo wa kuwapokonya silaha waasi wa Rwanda wa FDLR ulianza tarehe 30 mwezi Mei mwaka huu chini ya usimamizi wa jamii ya kimataifa,Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(Sadc).

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!