Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » JE,ULIKISOMA KILE AMBACHO UMOJA WA MATAIFA ULICHO KISEMA KUHUSU HALI YA USALAMA WA IRAQ?

JE,ULIKISOMA KILE AMBACHO UMOJA WA MATAIFA ULICHO KISEMA KUHUSU HALI YA USALAMA WA IRAQ?

Written By Unknown on Thursday, 14 August 2014 | Thursday, August 14, 2014

Umoja wa Mataifa umesema kuwa mgogoro wa kibinadamu nchini Iraq ni wa kiwango cha juu sana, huku mamia ya maelfu ya wananchi wa nchi hiyo wakiendelea kukimbia makazi yao kutokana na mashambulizi ya kundi la kigaidi la Daesh.
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Nickolay Mladenov amesema kwamba, kutangaza hali hiyo ya dharura kunahitajia kuanza kupelekwa misaada ya ziada na fedha ili kukidhi mahitaji ya watu waliokimbia makazi yao.

Mgogoro wa Iraq umeshtadi katika wiki za hivi karibuni baada ya wanamgambo wa Daesh kudhibiti miji kadhaa ya kaskazini mwa nchi hiyo na kuwalazimisha Wakristo walio wachache na jamii ya Wakurdi wa Yazidi kuondoka majumbani kwao. Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, wakimbizi karibu 35,000 wengi wao wakiwa Wakurdi wa jamii ya Yazidi wamekimbilia katika eneo la Kurdistan la Syria katika siku 3 zilizopita.


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi