Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » UMOJA WA MATAIFA WAIOMBA SERIKALI YA SOMALIA KUUNDA HARAKA SAANA KAMATI YA UCHAGUZI.

UMOJA WA MATAIFA WAIOMBA SERIKALI YA SOMALIA KUUNDA HARAKA SAANA KAMATI YA UCHAGUZI.

Written By Unknown on Thursday, 14 August 2014 | Thursday, August 14, 2014

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wametaka kuuundwe kamati huru ya kitaifa kwa ajili ya kurekebisha katiba na kuandaa mazingira ya kufanyika uchaguzi wa rais nchini Somalia mwaka 2016.
Mark Lyall Grant, mwakilishi wa Uingereza katika UN ambaye pia ni mwenyekiti wa sasa wa Baraza la Usalama amesema alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mogadishu kwamba, lengo la safari ya ujumbe wa Baraza la Usalama nchini Somalia ni kutangaza uungaji mkono kamili wa Umoja wa Mataifa kwa wananchi wa nchi hiyo na kusaidia kufikiwa matakwa yao.
Vilevile emeeleza kuridhishwa kwake na mwenendo wa mabadiliko ya kisiasa katika miezi ya hivi karibuni nchini humo na kuwataka maafisa wa serikali ya Somalia kuunda haraka iwezekanavyo tume huru kwa ajili ya kufanya marekebisho katika katiba na kuitishwa kura ya maoni mwaka 2015 ili kuandaa mazingira ya kufanyika uchaguzi wa rais mpya wa Somalia mwaka 2016.
Ujumbe wa Baraza la Usalama uliotembelea Somalia umekutana na kufanya mazungumzo na Rais Hassan Sheikh Muhammad wa nchi hiyo, Waziri Mkuu Abduwali Sheikh Ahmad na baadhi ya maafisa wa ngazi za juu na bunge wa Somalia.




TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi