Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa, mlipuko wa ugonjwa
wa homa ya Ebola hadi sasa umesabisha vifo vya watu 1,069 ambapo watu 56
miongoni wao walikufa siku mbili ziliopita.
Maambukizi mapya na vifo vimeripotiwa katika nchi za Magharibi mwa Afrika za Liberia, Sierra Leone, Guinea na Nigeria. Wakati huo huo Canada imesema kuwa itatoa dozi 1,000 za chanjo ya majaribio ya ugonjwa wa Ebola kwa shirika la Afya Duniani ili zitumike katika nchi za Afrika.
Hatua hiyo imetangazwa baada ya WHO kusema kuwa ni sawa kimaadili kutumiwa dawa hiyo ambayo bado inafanyiwa majaribio ili kutibu wagonjwa katika hali ya dharura. Chanjo hiyo imeonesha mafanikio katika uchunguzi wa mnyama lakini hata hivyo bado haijajaribiwa kwa mwanadamu. Hakuna tiba ya homa ya Ebola ambayo dalili zake ni kuharisha, kutapika na kutokwa damu katika sehemu mbalimbali mwilini.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!