Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , , » SOMA KILE CHOTE ULIKUWA HAUJUI KUHUSIANA NA NDOWA YA MA STAR WAWILI WA AFRICA MASHARIKI AMBAO NI WEMA SEPETU NA MWANAMUZIKI DIAMOND.

SOMA KILE CHOTE ULIKUWA HAUJUI KUHUSIANA NA NDOWA YA MA STAR WAWILI WA AFRICA MASHARIKI AMBAO NI WEMA SEPETU NA MWANAMUZIKI DIAMOND.

Written By Unknown on Saturday 23 August 2014 | Saturday, August 23, 2014

Msanii asiye isha vituko na ambae amejijengea jina kwa muda mfupi nakuonekana kuwa ghali zaidi nchini Tanzania kwa sasa, ametamka hayo alipozungumza na Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam juzi Jumatano.
Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo, ikiwemo maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo.
“Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo mambo yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie,” alisema Diamond.


Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.
“Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza.
“Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka haraka kwa sababu wengi nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya Instagram,tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.”

Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri waswahili wanasema lazima uvifiche, hata Mwenyezi Mungu naye anasema anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa. Wakati mwingine kunakuwa na husda,hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi saana vinaweza kutofanikiwa.”
Taarifa kwamba Diamond hataoa zilisambaa na kudaiwa kumchefua mchumba wake Wema Sepetu ambapo katika mahojiano mkali huyo wa ‘Mdogo Mdogo’ alisema: “Kwanza sikuwahi kusema kwamba siwezi kuoa, nilishtushwa na gazeti hilo, nilisikitika kwa kweli na iliniuma sana, lakini nikaona nikijibu nitaonekana kwamba sina adabu, kwa sababu siku zote anayeanza huwa haonekani lakini anayemaliza. Pia siwezi kubishana na vyombo vya habari, mwisho wa siku ni watu haohao nitawategemea wanifanyie kazi zangu,” alisema Diamond.
Hata hivyo Diamond alisema mchumba wake anaumizwa na vichwa vya habari ambavyo vimekuwa mwiba kwake.
“Hata hivyo magazeti yetu tumeshayazoea jinsi yanavyoandika, wakati mwingine inakuwa kama chachandu au kufurahisha baraza,” aliongeza.
Kuhusu taarifa kwamba ameachana na mchumba wake huyo, alisema: “Hatuna tatizo watu wengi wanasema tumeachana, lakini hatujaachana na hatuwezi kujibishana.
“Sijui nikujibu nini kwa sababu kila nitakachokujibu utaona namsifia kwa sababu yule ni mchumba wangu.
“Lakini ninachoweza kukwambia ni kuwa sisi ndio tunaoujua ukweli wa uhusiano wetu.
“Sidhani kama ni sahihi mapenzi yetu yakawa na wasemaji wengine zaidi yetu wenyewe. Sasa ni ajabu watu wanaposema yao"


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi